1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

CDU yatabiriwa ushindi uchaguzi wa jimbo kubwa Ujerumani

15 Septemba 2025

Chama cha Kansela wa Ujerumani cha Christian Democratic Union (CDU), kinaelekea kupata ushindi katika uchaguzi wa jimbo muhimu la North Rhine-Westphalia (NRW) uliofanyika siku ya Jumapili.

https://p.dw.com/p/50Szr
Ujerumani, Cologne, 2025 | Mabango ya kampeni
Uchaguzi kwenye jimbo la North-Rhein Westphalia unazingatiwa kuwa kipimo kwa umashuhuri wa chama cha CDU na Kansela Friedrich Merz.Picha: Manngold/IMAGO

Matokeo ya awali yanaonesha chama hicho cha Kansela Friedrich Merz kitajikingia hadi asilimia 33.7 ya kura kikifuatiwa na chama cha Social Democratic Party (SPD) kitakachopata asilimia 22.1 ya kura. 

Chama cha mrengo mkali wa kulia cha AfD kitaambulia asilimia 15 pekee ambayo hata hivyo ni ongezeko la asilimia 5 ikilinganishwa na uchaguzi wa mwaka 2020.

Vyama vingine ikiwemo kile cha kijani (Die Grünne) na FDP vimepata matokeo mabaya. Uchaguzi kwenye jimbo hilo lenye wakaazi wengi zaidi nchini Ujerumani unazingatiwa kuwa kipimo cha umashuhuri binafsi na wa chama cha Kansela Merz aliyeingia madarakani mwezi Mei mwaka huu.