CAIRO: Kansela wa Ujerumani Angela Merkel aanza ziara ya Mashariki ya Kati. | Habari za Ulimwengu | DW | 04.02.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

CAIRO: Kansela wa Ujerumani Angela Merkel aanza ziara ya Mashariki ya Kati.

Kansela wa Ujerumani, Bibi Angela Merkel, ameanza ziara yake ya siku nne Mashariki ya Kati kwa mashauriano na Rais wa Misri, Hosni Mubarak, mjini Cairo.

Viongozi hao wamesisitiza haja ya mkakati wa pamoja wa kimataifa kufufua mashauriano ya amani kati ya Israil na Wapalestina.

Bibi Angela Merkel ameipongeza Misri kwa jitihada zake ambazo hazijafanikiwa za kuvipatanisha vyama hasimu vya Wapalestina.

Kansela huyo wa Ujerumani anatarajiwa pia kuzitembelea Saudi Arabia, Muungano wa Mataifa ya Kiarabu, na Kuwait.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com