1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Mkutano wa kupambana na uhamiaji wafanyika mjini Dresden

15 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCaN

Mawaziri wa mambo ya ndani wa nchi za Umoja wa Ulaya wanakutana mjini Dresden mashariki mwa Ujerumani kujadili njia za kuboresha ushirikiano katika kukabiliana na tatizo la wakimbizi haramu barani Ulaya.

Kamishna wa halmashauri ya Umoja wa Ulaya anayehusika na sheria na maswala ya ndani, Franco Frattini, anatarajiwa kutumia mkutano huo kuwataka wanachama wote wa Umoja wa Ulaya kutoa boti na ndege za kusaidia kazi ya kushika doria kwenye bahari ya Mediterenia.

Maelfu ya wahamiaji hujaribu kuingia Ulaya kila mwaka kupitia bahari ya Mediterenia wakitokea eneo la kaskazini mwa Afrika.

Mawaziri hao wanataraji wa pia kujadili pendekezo la Umoja wa Ulaya la kutoa vibali rasmi vya kuishi Ulaya ili kuwavutia wahamiaji wenye ujuzi wa hali ya juu kikazi katika umoja huo.