BERLIN: Mbunge wa chama cha CDU apinga Marekani kuiuzia silaha Saudi Arabia | Habari za Ulimwengu | DW | 30.07.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BERLIN: Mbunge wa chama cha CDU apinga Marekani kuiuzia silaha Saudi Arabia

Mbunge wa chama cha Christian Democratic hapa Ujerumani, Ruprecht Polenz, ameikosoa mipango ya Marekani kuiuzia silaha Saudi Arabia na nchi nyengine za Mashariki ya Kati.

Kwenye mahojiano yake na gazeti la Frankfurter Rundschau, mwenyekiti huyo wa kamati ya bunge la Ujerumani inayoshughulikia sera za kigeni, ametaka badala yake juhudi zifanywe kukusanya silaha katika eneo hilo.

Mpango wa Marekani kuuza silaha zake Mashariki ya Kati unaonekana kuwa mkakati wa kutaka kuidhibiti Iran huku nchi hiyo ikiendelea kujiimarisha.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com