BERLIN: Majadiliano kati ya Marekani na Korea Kaskazini yamalizika | Habari za Ulimwengu | DW | 19.01.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BERLIN: Majadiliano kati ya Marekani na Korea Kaskazini yamalizika

Maafisa wa Marekani na Korea ya Kaskazini wamekamilisha majadiliano ya siku tatu katika mji mkuu wa Ujerumani Berlin.Majadiliano hayo yamehusika na mradi wa kinuklia wa Korea ya Kaskazini.Ingawa mpatanishi mkuu wa Marekani Christopher Hill hapo awali alisema mazungumzo hayo yalikuwa ya maana,hakueleza zaidi alipoondoka Berlin kuelekea Asia.Lakini alidokeza kuwa ni matumaini yake kuwa mazungumzo ya kundi la pande sita huenda yakafanywa hivi karibuni.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com