BERLIN: Bunge la Ujerumani limepitisha bajeti ya mwaka 2007 | Habari za Ulimwengu | DW | 25.11.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BERLIN: Bunge la Ujerumani limepitisha bajeti ya mwaka 2007

Bajeti ya mwaka 2007 imeidhinishwa na bunge la Ujerumani mjini Berlin.Katika bajeti hiyo, serikali itakuwa na deni jipya la Euro bilioni 19.6.Vitegauchumi vipya vitagharimu kama Euro bilioni 24 na kwa hivyo huambatana na sheria ya kikatiba kuwa jumla ya vitegauchumi iwe kubwa kuliko deni jipya.Mwishoni mwa mdahalo wa bunge, waziri wa fedha Peer Steinbrück alisema,hali ya kiuchumi iliyokuwa bora isiamshe matumaini yasioweza kutimizwa.Akaeleza kuwa matatizo ya kimsingi kuhusu matumizi ya serikali bado yapo pale pale.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com