Benazir azikwa huku ghasia katika sehemu za nchi zikiendelea | Habari za Ulimwengu | DW | 28.12.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Habari za Ulimwengu

Benazir azikwa huku ghasia katika sehemu za nchi zikiendelea

ISLAMABAD:

Huku mazishi ya Bi Benazir Butho alieuliwa alhamisi,yakiwa kusini mwa Pakistan, katika baadhi ya sehemu za nchi hiyo hali inazidi kuwa ya wasiwasi kufuatia wafuasi wake wenye hasira,kuendelea kushambulia majengo ya serikali pamoja na mali za watu binafsi.

Eneo ambalo limekumbw na ghasia nyingi ni jimbo la kusini la Sindhi ambalo ndio ngome ya Bhuto.Watu wapatao 20 wakiwemo polisi wameuawa tangu jana.

Watu wenye jazba wakupuuza mwito wa rais Musharraf wa kubaki watulivu, wameendelea kuchoma magari kadhaa huku wakirandaranda katika barabra ambazo zilikuwa hazina watu.

Aliekuwa zamani mtu wa karibu sana na Bi Benazir Bhuto- Husain Haqqan anagusia suala la lawama wengi wakisema serikaili ilishindwa kumpa Bi bhuto ulinzi wa kutosha.

Mazishi ya Bi Bhutto yamefanyika katika kijiji cha Garhi Khuda Baksh katika wilaya Larkana kusini mwa nchi hiyo.

Rais Musharraf ametangaza siku tatu za maombolezo.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com