BEIRUT : Jeshi laendelea kuzingira kambi ya wakimbizi | Habari za Ulimwengu | DW | 23.06.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BEIRUT : Jeshi laendelea kuzingira kambi ya wakimbizi

Jeshi la Lebanon limesema linaendelea na operesheni za kijeshi zenye lengo la kuwatokomeza wapiganaji waliobakia wa kundi la Fatah Al –Islam kwenye kambi ya wakimbizi wa Kipalestina ya Nahr al- Bared kaskazini mwa Lebanon.

Waziri wa ulinzi wa Lebanon amesema hapo mapema kwamba wanamgambo hao wa Kiislam waliojichimbia kwenye kambi hiyo wameshindwa na kwamba jeshi hivi sasa limekuwa likijishughulisha na operesheni ya kusafisha masalia ya wanamgambo hao.

Maelfu ya wakimbizi wa Kipalestina inasemekana kuwa wameendelea kubakia kusini mwa kambi hiyo.Watu 170 wameuwawa wakiwemo wanajeshi 80 wa Lebanon katika mapigano yaliodumu kwa zaidi ya mwezi mmoja.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com