Beirut. Bomu latupwa dhidi ya nyumba moja karibu na jengo la UM.
15 Oktoba 2006Matangazo
Kiasi watu wanne wamejeruhiwa katika shambulio dhidi ya nyumba moja iliyoko karibu na jengo la umoja wa mataifa katika mji mkuu wa Lebanon Beirut.
Msemaji wa wizara ya mambo ya ndani nchini Lebanon amesema kuwa bomu la kutupwa kwa mkono lilirushwa mapema asubuhi dhidi ya nyumba hiyo , ambayo iko karibu pia na hoteli.
Wiki iliyopita kulifanyika shambulio kama hilo la bomu dhidi ya kituo cha polisi mjini Beirut.
Hakuna mtu aliyejeruhiwa katika tukio hilo, na pia hakuna taarifa za sababu zilizopelekea kufanyika shambulio hilo.