BEIJING: Mazungumzo ya mataifa sita yamalizika bila makubaliano kufikiwa | Habari za Ulimwengu | DW | 22.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BEIJING: Mazungumzo ya mataifa sita yamalizika bila makubaliano kufikiwa

Wajumbe wa Marekani katika mazungumzo ya mataifa sita wameitaka Korea Kaskazini kuyapa umuhimu mkubwa mazungumzo hayo kufuatia majadiliano ya wiki nzima ambayo hayakufaulu kufikia makubaliano kuhusu mpango wa nyuklia wa Korea Kaskazini.

Mjumbe maalumu wa Marekani katika mazungumzo hayo, Chistopher Hill, leo ameelezea wasiwasi wake ikiwa kutapatikana makubaliano.

Serikali ya Pyongyang imeitaka Marekani ionde vikwazo vyake vya kifedha dhidi yake pamoja na kufunguliwa kwa akaunti za benki zilizofungiwa.

Wakati haya yakiarifiwa, waziri wa mashauri ya kigeni wa Marekani, Condoleezza Rice, amesisitiza mjini Washington kwamba maswala ya fedha hayapaswi kuzungumziwa sambamba na mpango wa nyuklia wa Korea Kaskazini.

Korea Kusini, Korea Kaskazini, Marekani, China Urusi na Japan zimeshiriki katika mazungumzo hayo yalioanza mnamo Jumatatu wiki hii baada ya kukwama kwa mwaka mmoja.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com