BAGHDAD: Al-Qaeda yadai kuhusika na mauaji ya Abu Reesha | Habari za Ulimwengu | DW | 15.09.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BAGHDAD: Al-Qaeda yadai kuhusika na mauaji ya Abu Reesha

Tawi la mtandao wa kigaidi wa Al-Qaeda nchini Irak limesema kuwa lilifanya shambulizi lililomuuwa kiongozi mashuhuri wa Kisunni,Abdul Sattar Abu Reesha katika Wilaya ya Al-Anbar.Abu Reesha alikuwa akiongoza kundi linaloshirikiana na majeshi ya Marekani kupambana na magaidi wa Al-Qaeda katika wilaya ya Anbar.

Juma lililopita,Rais wa Marekani,George W.Bush alikutana na Abu Reesha,alipofanya ziara yake ya ghafula nchini Irak.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com