1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Afrika Kusini kutohudhuria mikutano ya G20 2026

4 Desemba 2025

Afrika Kusini imesema iko tayari kusubiri kutohudhuria mikutano ya kundi la nchi tajiri na zinazoinukia kiuchumi za G20 mwaka 2026 baada ya kuzuiwa na Marekani na haikuratajia nchi nyingine kushawishi ili ishirikishwe.

https://p.dw.com/p/54k1T
Cape Town, Afrika Kusini 2025 | G20
Mkutano wa Kilele wa G20 mwaka 2025 ulifanyika Afrika Kusini Picha: Kyodo/picture alliance

Hayo yameelezwa Alhamisi na msemaji wa serikali, Vincent Magwenya akisema kwamba Afrika Kusini haitoshiriki mikutano kadhaa ya G20 ya mwaka 2026 na itarejea tena wakati urais wa G20 utakapokabidhiwa kwa Uingereza mwaka 2027.

Magwenya ameandika katika mtandao wa kijamii kwamba kwa sasa watapumzika kwa muda hadi watakaporejea tena katika programu za kawaida.

Marekani yachukua urais wa mwaka mmoja

Amesema Afrika Kusini haikutarajia nchi nyingine za G20 kuususia urais wa Marekani au kushawishi ijumuishwe.

Mwezi huu, Marekani imechukua urais wa mwaka mmoja wa G20, baada ya kususia kwa kiasi kikubwa mikutano ya Afrika Kusini, ukiwemo ule wa kilele uliofanyika mwezi Novemba mjini Pretoria.