1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Abbas ageuza sheria ya uchaguzi

2 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBTI

RAMALLAH:

Rais Mahmoud Abbas wa Palestina ametangaza leo mageuzi katika sheria ya uchaguzi ikiwa na shabaha ya kuimarisha chama chake cha FATAH dhidi ya kile cha hasimu wake Hamas.hii ni hatua mpya ya rais Abbas kukitenga chama cha Hams tangu chama hicho chenye msimamo mkali kunyakua madaraka kwa nguvu katika mwambao wa Gaza hapo juni.

Abbas amekitimua chama cha Hamas nje ya serikali ya Palaestina,ingawa ndicho kilichoshinda uchaguzi.Hakujawekwa bado tarehe ya uchaguzi mpya.