1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zaidi ya watu 250 wafa kufuatia kimbunga Nargis nchini Myanmar

4 Mei 2008

-

https://p.dw.com/p/DtLH

YANGON

Serikali ya kijeshi ya Myanmar imetangaza hali ya dharura katika majimbo matano yaliyokumbwa na uharibifu mkubwa kutokana na kimbunga Nargis. Vyombo vya habari nchini humo vimeripoti kwamba zaidi ya watu 250 wamekufa katika mji mkuu Yangon kufuatia kimbunga hicho kilichotokea jana.Kimbunga Nargis kiliaandamana na upepo mkali na kuharifu paa za nyumba na kuacha barabra za miji kadhaa nchini humo zikigubikwa na vifusi vya majengo yaliyoporomoka pamoja na miti iliyongoka.Wataalamu wa Umoja wa mataifa wanaohusika na masuala ya majanga ya dharura wamefahamisha kwamba itachukua muda wa siku kadhaa kabla ya kukadiriwa uharibifu uliofanywa na kimbunga hicho.Idadi ya watu waliouwawa inatazamiwa kupanda.