Zaidi ya 28 wafa Nigeria | IDHAA YA KISWAHILI | DW | 26.12.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

IDHAA YA KISWAHILI

Zaidi ya 28 wafa Nigeria

---

ABUJA

Takriban watu 28 wameuwawa baada ya bomba la mafuta kushika moto mjini Lagos hapo jana.Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na shirika la msalaba mwekundu nchini humo watu hao walikuwa wakijaribu kuiba mafuta katika bomba hilo lililokuwa likivuja.

Wafanyikazi wa shirika la msalaba mwekundu bado wako katika hilo la mkasa kuwaokoa baadhi ya watu ambao wamejeruhiwa huku idadi ya waliokufa ikitarajiwa kuongezeka.

Matokeo kama hayo yamekuwa yakiripotiwa mara nyingi nchini humo.mwezi wa Desemba mwaka jana zaidi ya watu 250 walikufa katika tukio kama hilo kwenye mji huo wa Lagos.Katika tukio la leo msemaji wa polisi amenukuliwa akisema watu 34 hadi sasa wamekufa huku taarifa za RedCross zikisema maiti 45 zimepatikana.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com