1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wawakilishi wa Hamas waondoka Kairo

Hawa Bihoga
30 Aprili 2024

Wawakilishi wa kundi la Hamas wameondoka mjini Kairo hivi leo, baada ya mazugumzo na maafisa wa Misri juu ya pendekezo jipya la makubaliano ya kusitisha mapigano.

https://p.dw.com/p/4fLUK
Khalil al-Hayya
Mwakilishi wa Hamas kwenye mazungumzo ya kusaka usitishaji mapigano, Khalil Al-Hayya.Picha: Khalil Hamra/AP Photo/picture alliance

Kituo cha televisheni cha Al-Qahira chenye mafungamano na serikali ya Misri kilisema ujumbe huo wa Hamas ungelirejea mjini humo ukiwa na majibu ya maandishi kwa pendekezo hilo, ingawa hakikutaja muda maalum. 

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Antony Blinken, alitazamiwa kuwasili nchini Israel ikiwa sehemu ya ziara yake kwenye eneo hilo iliyoanzia jana nchini Saudi Arabia. 

Soma zaidi: Blinken airai Hamas kuridhia ombi la Israel kuwaachia mateka

Waziri huyo, ambaye nchi yake ni mshirika mkubwa wa utawala wa Israel, alisema serikali mjini Tel Aviv inapaswa kufanya mengi zaidi katika kuruhusu misaada kuingia kwenye Ukanda wa Gaza, lakini jambo bora zaidi ni kwa pande hizo kufikia makubaliano ya kusitisha mapigano.