Watu wasiopungua 80 wafa kutokana na mafuriko pamoja na maporomoko ya ardhi Indonesia | Habari za Ulimwengu | DW | 28.12.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Habari za Ulimwengu

Watu wasiopungua 80 wafa kutokana na mafuriko pamoja na maporomoko ya ardhi Indonesia

JAKARTA:

Watu wasiopungua 87 wameuawa na maelfu kadhaa kuachwa bila makazi kufuatia msururu wa maporomoko ya ardhi na mafuriko katika sehemu za mashambani nchini Indonesia.

Barabara nyingi hazipitiki kutokana na daraja kuwa zimevunjika ama kufunikwa na udongo hivyo magari makubwa ambayo yangetumiwa kwa uokozi kushindwa kufika yanakohitajika.

Mvua mabyo imkuwa ikinyesha kwa siku kadhaa imesababisha mito kufurika,huku maporomoko ya ardhi yapatayo saba kufunika vijiji kadhaa na kuharimu nyumba za katika wilaya ya Karanganyar katikati ya eneo la Java.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com