Watu 150 wazama baharini wakikimbilia Ulaya | Habari za Ulimwengu | DW | 11.12.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Watu 150 wazama baharini wakikimbilia Ulaya

Hadi watu 150 wamepoteza maisha yao baharini katika ajali tatu za boti,walipojaribu kukimbilia Ulaya.Zaidi ya watu 50 walifariki baada ya boti iliyotokea Mauritania na kuelekea Visiwa vya Canary kuzama katika Bahari ya Atlantik.Wengine 51 walizama nje ya mwambao wa Uturuki baada ya boti iliyojaa watu kupinduka katika Bahari ya Aegean karibu na Izmir.Kama Waafrika 59 pia walizama baharini kaskazini mwa mji mkuu wa Senegal,Dakar.

Mwaka uliopita,baada ya kuimarishwa kwa ulinzi wa mwambao,idadi ya watu waliowasili katika Visiwa vya Canary nchini Hispania,ilipunguka kwa asilimia 60.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com