Watoto wapatao 19 wafariki kwenye sherehe ya Sikukuu ya Idd El Fitr huko Tabora nchini Tanzania | Masuala ya Jamii | DW | 02.10.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Masuala ya Jamii

Watoto wapatao 19 wafariki kwenye sherehe ya Sikukuu ya Idd El Fitr huko Tabora nchini Tanzania

Nchini Tanzania katika mkoa wa Tabora, watoto wapatao 19 wamefariki hapo jana kutokana na msongamano kwenye ukumbi wa disco wakati walipokuwa kwenye shamrashamra za sikukuu ya Eid el fitri.

Watoto hao walikuwa na umri kati ya miaka 12 na 17, ambapo wengine kadhaa wamejeruhiwa wawili kati yao wakiwa katika hali mbaya.

Hilo ni tukio baya kabisa kuwahi kutokea wakati wa kipindi cha sherehe za sikukuu hiyo ya Eid el Fitr katika historia ya Tanzania.

Ili kufahamu zaidi juu ya tukio hilo Aboubakary Liongo amezungumza na Mkuu wa Mkoa huo wa Tabora Abeid Mwinyimusa.

Sauti na Vidio Kuhusu Mada

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com