WASHINGTON:Jeshi la Iran kusajiliwa kwnye orodha ya makundi ya kigaidi | Habari za Ulimwengu | DW | 16.08.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

WASHINGTON:Jeshi la Iran kusajiliwa kwnye orodha ya makundi ya kigaidi

Marekani ina mpango wa kuliorodhesha kundi la kijeshi la Iran Revolutionary Guards katika orodha ya makundi ya kigaidi.

Hatua hiyo inayopewa umuhimu mkubwa wa kidiplomasia itasababisha matatizo ya kichumi kutokana na kuzuiwa mali na miamala ya fedha ya kimataifa.

Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa Marekani kuliorodhesha jeshi la nchi huru katika orodha ya makundi ya kigaidi.

Mwezi machi mwaka huu wanajeshi wa Revolutionary Guards waliwakamata askari wanamaji 15 wa Uingereza hatua iliyozusha mvutano kati ya Tehran na London.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com