WASHINGTON : Bush amtaka Musharaff kuitisha uchaguzi | Habari za Ulimwengu | DW | 08.11.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

WASHINGTON : Bush amtaka Musharaff kuitisha uchaguzi

Rais George W, Bush wa Marekani amezungumza kwa njia ya simu na Rais Pervez Musharaf wa Pakistan na amemhimiza kiongozi huyo kuachana na wadhifa wake wa mkuu wa majeshi na kuitisha uchaguzi haraka nchini humo wakati upinzani ukidai kwamba mamia wametiwa mbaroni wakati wa usiku kuzima maandamano makubwa dhidi ya hali ya hali ya hatari iliotngazwa nchini humo.

Bush amekuwa akishutumiwa kwa kutomshinikiza Musharraf baada ya mshirika huyo muhimu wa Marekani kutangaza utawala wa hali ya hatari na kuvunja maandamano kwa kutumia nguvu.

Mapema polisi walipambana na wafuasi wa Waziri Mkuu wa zamani wa Pakistan Benazir Bhutto mjini Islamabad wakati takriban watu 200 walipokuwa wakilikaribia bunge.Bhutto ametowa wito wa kufanika kwa maandamano hapo Ijumaa mjini Rawalpindi licha ya kupigwa marufuku kwa maandamano na serikali.Bhutto pia ametishia kuwakusanya wafuasi wake kwenye maandamano makubwa nchini kote venginevyo Musharraf anarudisha utawala wa katiba,anaitisha uchaguzi na kujiuzulu wadhifa wake wa mkuu wa majeshi.

Wakati huo huo Mwanasheria mkuu wa serikali Malik Qayum amesema uchaguzi wa bunge nchini humo yumkini ukafanyika mwezi wa Februari na hali ya hatari ikaondolewa hapo mwezi wa Desemba.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com