1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaNiger

Washauri wapya wa kijeshi wa Urusi wawasili Niger

6 Mei 2024

Washauri wapya wa kijeshi wa Urusi wamewasili nchini Niger pamoja na zana za kijeshi, kulingana na Televisheni ya taifa ya nchi hiyo inayotaka wanajeshi wa Marekani kuondoka.

https://p.dw.com/p/4fXbk
Utawala wa kijeshi wa Niger, ambao ulichukua mamlaka katika mapinduzi ya mwaka  2023, uliwafukuza wanajeshi wa Ufaransa na kisha kukatisha makubaliano ya ushirikiano wa kijeshi na Marekani.
Utawala wa kijeshi wa Niger, ambao ulichukua mamlaka katika mapinduzi ya mwaka  2023, uliwafukuza wanajeshi wa Ufaransa na kisha kukatisha makubaliano ya ushirikiano wa kijeshi na Marekani.Picha: Balima Boureima/picture alliance/AA

Kundi la kwanza la washauri 100 wa Urusi waliwasili Niger mnamo Aprili 10 pamoja na mifumo ya ulinzi wa anga.

Ripoti zinasema kwamba Urusi imetuma ndege tatu za shehena ya nyenzo za kijeshi na wakufunzi ndani ya kipindi cha mwezi mmoja uliopita.

Waziri wa ulinzi wa Marekani Lloyd Austin alidokeza wiki iliyopita kwamba wanajeshi wa Urusi sasa wamewekwa katika kambi ya wanaanga ya Niger karibu na uwanja wa ndege wa Niamey ambao pia una wanajeshi wa Marekani.

Utawala wa kijeshi wa Niger, ambao ulichukua mamlaka katika mapinduzi ya mwaka  2023, uliwafukuza wanajeshi wa Ufaransa na kisha kukatisha makubaliano ya ushirikiano wa kijeshi na Marekani.