Wafadhili kuwapa Wapalestina zaidi ya dola bilioni 7 | Habari za Ulimwengu | DW | 18.12.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Wafadhili kuwapa Wapalestina zaidi ya dola bilioni 7

PARIS

Wafadhili wa kimataifa wameahidi kuwapa Wapalestina dola bilioni 7.4 katika mkutano wao wa siku moja uliofanyika hapo jana mjini Paris Ufaransa.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Condoleeza Rice amesema michango hiyo ya fedha ni matumaini ya mwisho ya kuinusuru serikali ya Wapalestina isifilisike.Waziri Mkuu wa Wapalestina Salam Fayyad aikuwa ameomba rasmi kupatiwa dola bilioni 5.6 kusaidia kutimiliza mpango wake wa kuendeleza uchumi unaofanya kazi kwa ajili ya taifa la baadae la Wapalestina.

Hata hivyo mkuu wa operesheni wa Chama cha Kimataifa cha Msalaba Mwekundu kwa Mashariki ya Kati Beatrice Megevand Roggo akizunguza na kituo cha televisheni ya Kiarabu cha Al Jazeera amesema msaada wa fedha na kibin adamu pekee hauwezi kutatuwa matatizo ya Wapalestina.

Roggo anasema fedha pekee haziwezi kutatuwa tatizo msaada wa kibinaadamu pekee hauwezi kutatuwa tatizo kwamba hivi sasa wanakabiliwa na matatizo huko Gaza kuhusiana na ukweli kwamba hakuna tena uchumi katika ukanda huo.Hakuna biashara ya kuingiza wala kusafirisha nje bidhaa mbali na kuingizwa kwa bidhaa muhimu hakuna kitu kengine zaidi ya hicho.

Wakati huo huo kundi la wanamgambo wa Kipalestina la Hamas linalodhibiti Ukanda wa Gaza limeuita mkutano huo wa wafadhili kwa kimataifa kuwa ni njama ya hatari yenye lengo la kuwagawa Wapalestina.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com