Viongozi wakuu wa serikali mpya ya Kenya watembelea maeneo yaliyoathiriwa na ghasia kutokana na uchaguzi
25 Aprili 2008Matangazo
Hapo jana viongozi hao Rais Mwai Kibaki, Waziri Mkuu Raila Odinga na Makamu wa rais Kalonzo Musyoka, walikuwa katika eneo la Eldoreti ambako inaarifiwa ya kwamba Rais Kibaki na Makamu wake walizomewa na wananchi.
Leo hii viongozi hao wako katika wilaya ya Kipkelion ambako kuna zaidi ya watu 1000 wanaoishi katika mahema baada ya kuyakimbia makazi yao kutokana na ghasia hizo.
Aboubakary Liongo alizungumza na mwandishi wa habari wa Citizen anayefuatana na viongozi hao, Ngige Ngugi.