Viongozi wa Ulaya na Afrika walaumiwa na waandishi mashuhuri | Habari za Ulimwengu | DW | 04.12.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Viongozi wa Ulaya na Afrika walaumiwa na waandishi mashuhuri

Kundi la waandishi maarufu limewatuhumu viongozi wa Ulaya na Afrika kwa kuwa na uoga wa kisiasa kwa kutoyapa kipaumbe masuala ya Darfur na Zimbabwe katika ajenda ya mkutano wa kilele wa Umoja wa Ulaya na Afrika utakaofanywa Lisbon nchini Ureno.

Waandishi hao,ikiwa ni pamoja na Vaclav Havel,Ben Okri na washindi wa Tuzo ya Nobel Gunter Grass na Nadine Gordimer,wamewashutumu wanasiasa hao kuwa wanayapa kisogo mizozo mibaya kabisa ya kiutu duniani.Wamesema,Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe anawakandamiza wapinzani wake na anateketeza uchumi wa nchi hiyo.Viongozi hao vile vile wanalaumiwa kuwa suala la Darfur halikuwekwa katika ajenda ya mkutano wao mjini Lisbon.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com