VALENCIA: Mabadiliko ya hali ya hewa yaathiri zaidi nchi masikini | Habari za Ulimwengu | DW | 13.11.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

VALENCIA: Mabadiliko ya hali ya hewa yaathiri zaidi nchi masikini

Wataalamu wa kisayansi na wajumbe wa jopo la Kiserikali juu ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa IPCC kutoka nchi 145 wanakutana Valencia nchini Uhispania.Wataalamu hao wanashauriana njia za kupambana na tatizo la ongezeko la ujoto duniani.

Katibu Mtendaji wa IPCC,Yvo de Boer amesema, athari za mabadiliko ya hali ya hewa zimedhihirika.Akaongezea kuwa nchi masikini ndio zitaathirika vibaya zaidi na hata uhai wa baadhi ya watu upo hatarini.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com