1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani kuanza kudondosha misaada Ukanda wa Gaza

Saumu Mwasimba
13 Machi 2024

Waziri wa ulinzi wa Ujerumani Boris Pistorius ametowa ridhaa kwa jeshi la wanaanga la nchi hiyo kuanza kudondosha msaada wa mahitaji ya dharura katika Ukanda wa Gaza.

https://p.dw.com/p/4dSW5
Palestina| Israel
Wapalestina wakikimbia kuokota misaada inayodondoshwa kwa njia ya angaPicha: AFP

Waziri wa ulinzi wa Ujerumani Boris Pistorius ametowa ridhaa kwa jeshi la wanaanga la nchi hiyo kuanza kudondosha msaada wa mahitaji ya dharura katika Ukanda wa Gaza.

Soma: Meli ya misaada ya chakula imeanza safari kutoka Cyprus kuelekea Gaza

Ujerumani inajiunga na nchi kadhaa nyingine ambazo zimekuwa zikidondosha msaada kwa kutumia ndege kwenye eneo hilo la Wapalestina linalozingirwa na Israel.

Kwa mujibu wa shirika la habari la kijerumani,dpa,waziri huyo wa ulinzi amesaini leo amri  ya kulitaka jeshi la Ujerumani Bundeswehr kuratibu shughuli hiyo. Inaelezwa kwamba tayari mkuu wa jeshi la wanaanga Luteni jenerali Ingo Gerhartz ameshatowa kibali maalum cha kuruhusu udondoshaji huo wa msaada.

Ujerumani sasa inajiunga na Marekani na Ufaransa ambazo pia zinaendesha operesheni kama hiyo.