MigogoroUlaya
Ujerumani yaahidi kitita cha dola bilioni 2 kwa Ukraine
16 Oktoba 2025
Matangazo
Tangazo la msaada huo limetolewa na Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani Boris Pistorius mjini Brussels siku ya Jumatano baada ya kukutana na mwenzake wa Ukraine Denys Shmyhal.
Waziri Pistorius amesema wa Ujerumani utatumika kununua silaha za karibu dola milioni 500 kutoka Marekani na kuipatia Ukraine ikiwemo mifumo ya ulinzi wa anga, rada za kijeshi na makombora.
Wawili pia walitia saini mkataba wa kuongeza ushirikiano wa kiulinzi unaojumuisha masuala ya utafiti na maendeleo ya teknolojia.
Ahadi hiyo ya msaada wa kijeshi imetolewa katika wakati serikali mjini Kyiv imesema itahitaji angalau dola bilioni 120 kwa mwaka 2026 zitakazoisadia kuwa na uwezo wa kuendelea kukabiliana na Urusi.