1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani, Ufaransa na Poland kujadili masuala ya usalama

22 Mei 2024

Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Ujerumani Annalena Baerboc anatarajiwa kukutana na wenzake wa Ufaransa Stéphane Séjourné na Poland Radoslaw Sikor-ski katika mji wa Ujerumani wa Weimar kwa mazungumzo ya Usalama.

https://p.dw.com/p/4g8iF
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa Stéphane Séjourné
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa Stephane Sejourne wakati wa mkutano na waziri mkuu wa Lebanon huko BeirutFebruari 6, 2024.Picha: JOSEPH EID/AFP

Hayo ni kwa mujibu wa msemaji wa ofisi ya mambo ya nje ya Ujerumani iliyopo Berlin aliyeongeza kuwa masuala mengine yatakayopewa kipaumbele katika mazungumzo hayo ni  Vita vya Urusi na Ukraine, na muelekeo wa siku za usoni wa Umoja wa Ulaya pamoja na mzozo wa Mashariki ya kati.

Baerbock atakutana na wenzake baada ya kurejea nchini hii leo kutoka Ukrainealikotoa wito wa usaidi zaidi wa kimataifa kwa Ukraine. Viongozi wa Ujerumani, Ufaransa na Poland hukutana mara kwa mara chini ya mwamvuli wa muungano wa Weimar ulioundwa mwaka 1991.