Ujerumani na sura ya vyama | Matukio ya Kisiasa | DW | 28.02.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Kisiasa

Ujerumani na sura ya vyama

Sura ya vyama vya kisiasa Ujerumani yaanza kubadilika na chama cha mrengo wa shoto kabisa Link Partei kinazidi kupata nguvu.

Sura ya vyama vya Ujerumani kuanzia mrengo wa kulia hadi wa kushoto imo kubadilika.Chama cha mrengo wa shoto-LINK PARTEI ambacho hadi sasa kikiwakilishwa bungeni Ujerumani mashariki au katika ile ilikua sehemu ya kikominist ya Ujerumani,sasa pia kimetia mguu wake magharibi mwa Ujerumani.Vyama vya kisiasa vya asili na jadi vimelazimika sasa kusaka vyama vyenye sura nyengine ili kuundanavyo serikali za muungano.

Sura ya vyama vya kisiasa nchini Ujerumani inageuka: katika chaguzi za serikali za mikoa 3 mnamo muda wa wiki 4 zilizopita,chama hicho cha mrengo wa shoto kiliweza kukiuka kizingiti cha 5% cha kura ili kuingia bungeni.

Kwahivyo, sasa LINK PARTEI -chama cha mrengo wa shoto kinawakilishwa katika mabunge ya mikoa 10 kati ya yote 16 ya Ujerumani.

Kutokana na hali hii ya mambo, vyama vyengine vya kisiasa humu nchini vimelazimika navyo kujirekebisha na kutafuta washirika wao wa kuunda nao serikali pamoja.Katika jaribio hilo vinakumbana na shida mno kuvunja miko yao ya siku za nyuma.Swali linalozuka hapa ni je, mfumo wa kisiasa uliodumu nchini Ujerumani muda mrefu umeanza sasa kupepesuka na si imara tena ?

Kuna wanaosema hofu hizo ni za nini ? Kwani, Ujerumani imepiga hatua mbele kujiunga na sura ilio ya kawaida barani Ulaya.Kwamba kuna chama cha mrengo wa shoto zaidi kukikiuka chama cha kijamaa cha SPD ni jambo la kawaida katika nchi nyingi za ulaya.Kwani, katika baadhi ya nchi kuna pia vyama vya mrengo wa kulia zaidi kuliko vile vya kihafidhina vya Cristian democrats bungeni.Hii ni hali ambayo hadi sasa ilikua geni Ujerumani.Kwahivyo, sababu gani kutaharuki ?

Mfano unaotisha sana wa aina hii ni sura iliopo nchini Itali ambako mgawanyiko wa vyama vingi unalemaza wakati fulani hali ya kisiasa .Hii haiwezi kutokea Ujerumani kwavile kuna kizingiti cha 5% cha kura kwa chama kuweza kuingia bungeni na kuathiri siasa.

kilichobadilika ni yale mazowea ya miongo kadhaa iliopita kuwa yakitoka tu matokeo ya uchaguzi inafahamika ni vyama gani chama fulani kitaunda nacho serikali ya muungano na kipi n i mwiko.

Swali lilikuwa iwapo ingetosha kuwa na wingi bungeni wa kuunda serikali pamoja na chama cha CDU au FDP cha kiliberali au chama cha kijamaa cha SPD kuungana na kile cha walinzi wa mazingira cha kijani.

Sura hii sasa imebadiolika .Mara ya kwanza kuibuka sura hii mpya ya kuzorota ni baada ya uchaguzi mkuu wa shirikisho 2005.Swali lilikua kuunda serikali ya bendera ya Jamaica -yaani ya rangi nyeusi,kijani na manjano-bendera za vyama 3 au .Hii ikawahivyo, kwavile hakuna mojawapo kati yavyama hivyo 3 kilikua tayari kufunga ndoa na chama cha cha mrengo wa shoto kabisa -chama cha wakoministi wa zamani.Kuunda serikali ya mfumo wa bendera ya Jamaica hakujawezekana kwavile vyama 2 vidogo vya bendera hizo-kijani na manjano-walinzi wa mazingira na waliberali havisikizani.

Hali hii sasa takriban imeshasahauliwa ,kwani mwiashoe vyama vikuu vya CDU-wahafidhina na SPD-wajamaa wakaunda serikali kuu inayotawala sasa mjini Berlin.Serikali hii chji ni ya kanzela Angela Merkel, kinyume na hofu za awali inaendesha mambo sawa sawa.

Hivi sasa kuna kitandawili kikubwa kukifumbua huko Hessen kuhusu kuunda serikali ya muungano:Hivi sasa ni vigumu kama ilivyokua miaka 2 na nusu nyuma kuunda serikali ya muungano ya mfumo wa Jamaica ,kwavile chama cha FDP hakitaki na chama cha kijani hakiafiki mfumo mwengine.Muungano wavyama 2 vikuu hautakiwi na SPD .Kwa hali hii, mtetezi mkuu wa chama cha SPD bibi Andrea Ypsilanti ,ingawa hataki kuunda serikali na chama cha mrengo wa shoto kabisa ,lakini yutayari kuchaguliwa waziri-kiongozi kwa msaada wa chama hicho bungeni.

Baadae anataka kuunda serikali isio na wingi kati ya chama chake na kile cha kijani.Mashaka ni kwamba, kabla ya uchaguzi aliahidi wapigakura hangeshirikiana kwa aina yoyote na chama cha mrengo wa shoto cha Link partei.Ikiwa hatachukua hatua hiyo, basi waziri mkuu wa mkoa wa Hessen aliepata pigo katika uchaguzi atabakia madarakani mpaka ufumbuzi wa kitandawili hicho upatikane.

Swali linaloulizwa nchini Ujerumani ni kwanini kuna watu wanaostuka kwa kuwa tu chama cha mrengo wa shoto na wanaitisha kuwepo sheria mpya za uchaguzi na Ilhali kila kitu cha wezekana.

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com