Ufaransa haioni haja ya kupelekwa msaada zaidi Myanmmar | Habari za Ulimwengu | DW | 24.05.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Habari za Ulimwengu

Ufaransa haioni haja ya kupelekwa msaada zaidi Myanmmar

-

Ufaransa ambayo ni mkosoaji mkubwa wa serikali ya kijeshi ya Myanmmar imehoji iwapo kuna haja ya kupelekwa msaada zaidi nchini humo wakati wanajeshi wake pamoja na wamarekani na Uingereza wamezuiliwa kuingia nchini humo kusaidia wahanga wa kimbunga cha Nargis.Meli kadhaa za kijeshi kutoka nchi hizo tatu zikiwa na zimesheheni misaada pamoja na ndege za Helikopta ambazo zingeweza kufikia maeneo yaliyoharibiwa vibaya na kimbunga hicho zimezuiliwa katika pwani ya nchi hiyo kwa zaidi ya wiki moja.Utawala huo wa kijeshi umeomba msaada wa dolla billioni 11 kutoka jumuiya ya kimataifa ambayo itakuwa na mkutano wa wafadhili hapo kesho mjini Yangon kwa ajili ya kuisaidia nchi hiyo. Aidha wafanyikazi wa misaada wa kimataifa bado wanasubiri kuruhusiwa kuingia nchini humo licha ya tangazo la katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki Moon kwamba amefanikiwa kuushawishi utawala wa kijeshi wa nchi hiyo kuwaruhusu wafanyikazi hao wa misaada kuingia kuwasaidia wahanga.Wakati huohuo watu wamemaliza kupiga kura ya maoni juu ya katiba mpya katika maeneo ambayo yameathirika zaidi na kimbunga ambako zoezi hilo halikuweza kufanyika tarehe 10 mwezi huu. Hata hivyo maafisa wanasema tayari katiba hiyo imeshaidhinishwa na wingi mkubwa katika duru ya mwanzo na matokeo ya zoezi la leo kwenye jimbo la Irrawady Delta na Yangoon hayawezi kubadilisha kitu.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com