Uchumi wa Kenya kuzorota zaidi? | Matukio ya Kisiasa | DW | 29.04.2008
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Kisiasa

Uchumi wa Kenya kuzorota zaidi?

Utafiti waonyesha kwamba uchumi wa Kenya huenda usirejee kaawaida mwaka huu

Ghasia zilizotokea Kenya zasababisha kuzorota kwa uchumi

Ghasia zilizotokea Kenya zasababisha kuzorota kwa uchumi

Uchumi wa kenya umeanguka kutoka asilimia 7 mwaka jana hadi asilimia 3.8 mwaka huu.


Hali hii inasababishwa na matokeo ya uchaguzi wa disema mwaka uliopita ambayo yalizua ghasia za kikabili nchini humo.


Utafiti uliofanywa na wataalamu wa shirika la habari la Rueters unaonyesha kwamba makubaliano yaliyoafikiwa kufuatia mkataba wa kuunda serikali inayojumlisha upinzani ambayo iliapishwa mwezi huu hayatasababisha kukua kwa uchumi hadi katika viwango vya kawaida nchini humo.


Wadadisia na wafanyibiashara 5 kati ya 11 waliiohojiwa wamesema hawatarajii uchumi huo kukuwa haraka na kufikia hata azimio la chini kabisa la serikali ya Kenya.


Wengi walioshiriki katika utafiti huo walitabiri kwamba shilingi ambayo imepewa msukumo na toleo la hisa za kampuni ya Safaricom itashuka thamani kwa asilimia 5; hivyo ikimaanisha kwamba shilingi 64 zitabadilishwa kwa dola moja ifikapo mwishoni mwa mwaka huu.


Wengine wamesema hawaoni kama kutakuwa na mabadiliko yoyote katika viwango vya riba nchini humo. Hata hivyo mmoja wao alitabiri kuongezeka kwa riba kwasababu ya mfumuko wa bei ambao umefikia asili mia 22 mwezi machi.


Mkuu wa maswala ya uchumi Africa katika benki ya Standard Chatered Bi Razia Khan amesema licha ya kurejea kwa utulivu hasara iliyotokana na ghasia nchini humo pamoja na mfumuko wa bei duniani vitazuia uchumi wa nchi kurejea kawaida mwaka huu.


Ameongezea kwamba ongezeko la bei ya mafuta linaogeza balaa kwa mfuko wa fedha wa nchi hiyo ambao unaohitaji msaada.


Benki kuu ya Kenya inasema hali ya uchumi ya mwaka jana ilisababisha kuogezeka kwa dola bilioni 1.3 kutoka kwa dola milioni 674.


Wakati bei ya mafuta inasababisha kupanda kwa bei ya kununua bidhaa za nje njia mbili zinazoipatia nchi hiyo pesa za kigeni utali na kilimo zinaonekana zikizorota mwaka huu.


Utalii unatarajiwa kuipatia nchi hiyo shilingi bilioni 50 mwaka huu. Hiyo itakuwa imepungua kwa asili mia 23 ikilinganishwa na pato la utali la mwaka uliopita.


Shughuli za utalii zilipungua kwani watalii wengi waliopanga kuitembea nchi hiyo ya Africa Mashariki walikatiza safari zao katika msimu wa utalii baada ya ghasia zilizosababisha vifo vya watu 1,200.


Wataalamu wengi wanasema mazao ya kilimo yatapungua kwani wakulima wengi wadogo wadogo ni miongoni mwa watu laki tatu na hamsini walioachwa bila makao kutokana na ghasia hizo.


Bodi ya chai ya Kenya imesema kuwa uzalishaji war obo ya kwanza ya mwaka umepungua kwa asilimia 35 hadi kilo 70 milioni.Hadi kufikia jana shilingi 62 zimebadilishana kwa dola 1.


Mkurugenzi mkuu wa kampuni ya bidco Vimal Shah amesema shilingi hiyo imekuwa kutokana na hisa za safaricom lakini biashara ya hisa hizo itakapomalizika huenda shilingi ikashuka thamani tena mpaka Kenya ipate mapato ya hali ya juu ambayo hadi sasa hayaonekani. Ameongezea kwamba misaada ya hali ya juu ikitolewa na wadhamini basi huenda ikasaidia uchumi wa nchi hiyo.

 • Tarehe 29.04.2008
 • Mwandishi Mwakideu, Alex
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/Dqqn
 • Tarehe 29.04.2008
 • Mwandishi Mwakideu, Alex
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/Dqqn
Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com