Trump awataka washirika wake "wajitokeze" kusaidia vita
20 Machi 2026
Matangazo
Trump ameitetea operesheni ya Marekani dhidi ya Iraniliyowashangaza washirika wake na ametumia mkutano wake na Takaichi kuwashinikiza washirika hao wa Marekani barani Asia na Ulaya.
Rais huyo ametoa wito wa meli zaidi kutumwa na mataifamengine katika mlango bahari wa Hormuz uliofungwa na Iran, ili kusindikiza meli za mafuta kuvuka.
Trump awali alikuwa amesema kuwa Marekani haihitaji usaidizi wowote.
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya mkutano wake na Trump, Takaichi amesema amemueleza Trump msaada ambao katiba ya Japan inaikubalia nchi hiyo kuutoa na kutotoa katika mlango huo bahari wa Hormuz.