Takaichi akutana na Trump chini ya shinikizo kuhusiana na Ho
19 Machi 2026
Mazungumzo hayo katika ikulu ya White House yanafanyikabaada ya takaichi kukataa mwito wa Trump wa kusaidia katika kuufungua mlango bahari wa Hormuz.
Takaichi ambaye ndiye waziri mkuu wa kwanza mwanamke wa Japan anaizuru Marekani wakati ambapo Trump amewashambulia marafiki wa nchi yake barani Asia na Ulaya, kwa kukataa kusaidia katika kuufungua mlango bahari wa Hormuz ambao Iran imeufunga kama kulipiza kisasi kutokana na vita vya Marekani na Israel dhidi yake.
Takaichi aliungwa mkono pakubwa na Trump kuelekea ushindi wake mkubwa katika uchaguzi wa Japan, ila kwa sasa anakabiliwa na changamoto kubwa ya kutotaka kumghadhabisha Trump katika wakati ambapo uchumi wa Japan unakabiliwa na athari za vita dhidi ya Iran ambavyo nchi hiyo haijahusika kuvianzisha.