BiasharaJapan
Japan yaikamata meli ya China na kuongeza uhasama baina yao
13 Februari 2026
Matangazo
Taasisi ya Uvuvi ya Japan imethibitisha kuikamata meli hiyo na kusema nahodha aliamriwa kusimama kwa ajili ya kukaguliwa na wakaguzi wa uvuvi, lakini alipuuza amri hiyo.
Meli hiyo ilikuwa na watu kumi pamoja na nahodha.
Ingawa Japan ikiwa ilizikamata meli za Korea Kusini na Taiwan katika miaka ya karibuni, lakini kisa hiki ni cha kwanza kinachohusisha meli kutoka China, tangu mwaka 2022.
Na ni kisa kinachojitokeza katikati ya mvutano wa kidiplomasia kati ya China na Japan, ulioanza mwezi Novemba baada ya kiongozi mpya wa Japan mhafidhina Sanae Takaichi kuashiria kwamba shambulizi lolote dhidi yao linaweza kuchochea hatua ya kijeshi.