1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaJapan

Msuguano kati ya China na Japan wazidi kuongezeka

9 Januari 2026

Mataifa hayo mawili makubwa ya Asia yameingia kwenye mvutano uliosababishwa na kauli ya Waziri Mkuu wa Japan, Sanae Takaichi, kuhusu changamoto za kiusalama zinazohusiana na Taiwan.

https://p.dw.com/p/56bN9
Korea Kusini Gyeongju 2025 | Sanae Takaichi akutana na Xi Jinping katika mkutano wa kilele wa Japani na China
Kwa muda mrefu China na Japan zimekuwa kwenye mgongano kuhusu masuala mbalimbaliPicha: Japan Pool/Jiji Press/AFP

Mvutano kati ya China na Japan unazidi kuongezeka kuhusu marufuku ya usafirishaji wa bidhaa zinazoweza kutumika kijeshi na kiraia. Mataifa hayo mawili makubwa ya Asia yameingia kwenye mvutano uliosababishwa na kauli ya Waziri Mkuu wa Japan, Sanae Takaichi, kuhusu changamoto za kiusalama zinazohusiana na Taiwan.

China inaiongezea Japan shinikizo la kiuchumi na kisiasa, pale ilipotangaza marufuku dhidi ya usafirishaji wa bidhaa kwa matumizi ya kijeshi na kiraia ikiwemo madini adimu.

Siku iliyofuata, Beijing ilianzisha uchunguzi kuhusu marufuku ya kemikali katika kiwanda cha Japan kinchotengeneza vifaa kama ‘semiconductors'.

Hatua hizo zilijiri muda mfupi baada ya China kufuta ziara ya ujumbe wa viongozi wa kibiashara wa Japan iliyopangwa mwezi huu.

China pia inatia shinikizo kwenye mashirika ya usafiri wa ndani, kufuta safari za Kwenda Japan. Hali ambayo imesababisha mamilioni ya Wachina kubadilisha safari zao kwa miezi ijayo.

Mgogoro huu umekua kwa takriban miezi miwili tangu Sanae Takaichi alipoeleza bungeni kwamba tukio la "kimkakati" la kijeshi dhidi ya Taiwan, linalotafsiriwa kama uvamizi wa China, linaweza kuathiri usalama wa Japan kwa kiwango kinachoweza kuhitaji majibu ya kijeshi.

China Pingtan 2025 | Meli ya China karibu na Kisiwa cha Pingtan, karibu na Taiwan
Waziri Mkuu wa Japan Sanae Takaichi adai hatua za China kudai udhibiti na umiliki wa Taiwan inaweza kuathiri usalama wa JapanPicha: Adek Berry/AFP/Getty Images

China, ambayo inaona Taiwan kuwa sehemu ya nchi yake, imeeleza kwamba maoni hayo ni mwingiliano usiofaa katika masuala yake ya ndani. Imeapa kuirudisha hata kwa nguvu ikihitajika.

Ongezeko la bajeti ya ulinzi wa Japan laipa China wasiwasi

China pia imeelezea wasiwasi wake kuhusu makadirio ya bajeti ya ulinzi ya Japan ambayo mwezi Disemba iliongezeka mara 3.8 na inatarajiwa kufika yeni trilioni 9 sawa na dola bilioni 49.2.

Hii imetafsiriwa na wachambuzi wengi kuwa ni kielelezo cha mwelekeo wa kujidhibiti kijeshi na kuongeza nguvu za kivita.

Kulingana na wachambuzi, akiwemo Ben Ascione, mhadhiri msaidizi wa Sias ana Mahusiano ya Kimataifa katika chuo kikuu cha Waseda mjini Tokyo, wasiwasi uliopo ni kwamba hakuna upande wowote ulio tayari kulegeza msimamo katika mgogoro huo. Wanahofia kwamba uhusiano kati yao unaweza kudorora zaidi.

Waziri Mkuu Takaichi hajaonyesha utayari wa kubadilisha au kuondoa maoni yake kuhusu Taiwan. Kwa upande mwingine Rais Xi Jinping ameiambia DW kwamba ana sababu thabiti za nyumbani zinazomzuia kulegeza msimamo.

Hii ina maanisha huenda Rais Xi Jinping atatafuta njia zaidi mbadala za kuilazimisha Japan kulegeza msimamo katika mgogoro wa sasa.

China na Japani zimekuwa zikigongana kwa muda mrefu juu ya masuala mengi, kuanzia uvamizi mkali wa Japan ya kikoloni katika miaka ya 1930 na ukatili wake kwa watu wa China, mizozo ya mipaka na ya kijeshi miongoni mwa mengine.