1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Takaichi aapishwa tena kama Waziri Mkuu wa Japan

19 Februari 2026

Sanae Takaichi ameapishwa tena kama waziri mkuu wa Japan, siku kumi baada ya ushindi wake mkubwa na wa kihistoria katika uchaguzi nchini humo.

https://p.dw.com/p/590gE
Sanae Takaichi, Waziri Mkuu wa Japan
Sanae Takaichi, Waziri Mkuu wa JapanPicha: Franck Robichon/REUTERS

Takaichi ameahidi kuuinua uchumi na kuimarisha ulinzi wa Japan ili kuilinda mipaka na bahari yake jambo ambalo huenda likaharibu uhusiano zaidi na China.

Mnamo Novemba iliyopita, Takaichi aliighadhabisha China kwa kusema huenda Japan ikaingilia kati kijeshi iwapo China itaichukua Taiwan kwa nguvu.

Waziri mkuu huyo wa Japan mwenye umri wa miaka 64,alikuwa waziri mkuu wa kwanza mwanamke wa nchi hiyo mnamo Oktoba na alishinda thuluthi mbili ya kura za wingi kwa chama chake katika uchaguzi ulioitishwa mapema bungeni mnamo Februari 8.

Amesema ushindi huo mkubwa alioupata unaonesha kuwa raia wa Japan wanataka mabadiliko muhimu ya kisera.