Takaichi, Trump kuangamiza zana za nyuklia Korea Kaskazini
28 Oktoba 2025
Takaichi amesema viongozi hao wawili wamekubaliana hayo katika mkutano wa kilele leo huko mjini Tokyo.
Takaichi na Trump vile vile wamesisitiza umuhimu wa amani Taiwan ingawa amekataa kutoa tamko lolote juu ya walichokijadili kuhusu China kwa sababu Trump atakutana na Rais wa China hivi karibuni.
Haya yanafanyika wakati ambapo mtu mmoja anayetuhumiwa kumuua kwa kumpiga risasi waziri mkuu wa zamani wa Japan Shinzo Abe miaka mitatu iliyopita, leo amekiri kumuua kiongozi huyo, wakati kesi dhidi yake ilipokuwa ikisikilizwa kwa mara ya kwanza.
Tetsuya Yamagami mwenye umri wa miaka 45 alikamatwa katika eneo la tukio hilo Julai 2022 baada ya kudaiwa kumfyetulia risasi Abe aliyekuwa anahutubia umati wa watu wakati wa kampeni za uchaguzi katika mji wa magharibi wa Japan wa Nara.