1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Trump adai kushinda asipoibiwa na chama cha Democratic

Sudi Mnette
6 Novemba 2020

Rais Donald Trump wa Marekani ametoa madai ya kufanyiwa wizi katika uchaguzi mkuu wa taifa hilo pasipo na kuwa na ushaihidi wowote.

https://p.dw.com/p/3kw22
US-Wahlen 2020 | Donald Trump Rede
Picha: Carlos Barria/Reuters

Rais huyo amesema mahasimu wake chama cha Democratic, wanafanya jaribio la wizi katika uchaguzi huo ambao alidai yeye anaweza kushinda kwa urahisi kabisa dhidi ya Joe Biden. Akizungumza katika Ikulu ya Marekani na kunukuliwa na vyombo kadhaa vya habari alisika akisema "Kama ukihesabu kura halali, nitashinda kwa wepesi.

Lakini kama utahesabu kura zisizo halali, wanaweza kutuibia uchaguzi huu." Hadi wakati huu timu ya kiongozi huyo imeanzisha kiasi kwa kiwango kikubwa cha madai katika lengo la kukabiliana kile alichokiita "ufisadi" wa chama cha Democrat. Hata hivyo maafisa katika baadhi ya majimbo ya uchaguzi bado hayajatoa uamuzi kuhusu malalamiko hayo.

Msingi wa madai ya Trump unajikita katika kura za kwa njia ya posta

US Wahl 2020 | Briefwahl in Florida
Karataisi za kupigia kura za MiamiPicha: Chandan Khanna/AFP/Getty Images

Bila shaka malalamiko ya Rais Trump yamejikita katika uhalali wa idadi kubwa za kura za awali zilizopigwa kwa njia ya posta, zaidi ya zile ambazo zilihusisha watu kwenda kupiga moja kwa moja katika siku ile ya uchaguzi ya Novemba 3. Kulikuwa idadi kubwa ya kura ambazo zilipigwa katika kuepusha maambukizi ya janga la corona ambalo limekwisha sababisha vifo vya zaidi ya watu 230,000 nchini Marekani.

Na kwa vile Trump alipuuza athari za janga la corona mara zote Trump aliwaambia wafuwasi wake wakapige kura moja kwa moja na wasiunge mkono utaratibu huo wa barua. Kwa hivyo idadi dongo ya wafuwasi wa chama chake cha Republican walishiriki zoezi hilo ukilinganisha na wale wa Democrat. Baadhi ya televisheni nchini Marekani zilisitisha kuonesha zoezi la kuhesabu kura la moja kwa moja ili kutoa fursa kwa wasimamizi wa uchaguzi kuyatolea ufafanuzi madai ya Trump. Katika duru ya uchaguzi kwa kura za majimbo Biden anaonekana yuko mbele kwa kura 264 na Trump 214.

Mnyukano wa Trump na Biden majimboni

US Wahl 2020 | Wahllokal in Colorado | Auszählung
Zoezi la kuhesabu kura katika eneo la DenverPicha: Chet Strange/AFP/Getty Images

Lakini pia katika maeneo ya kuhesabu kura kama jimbo la Pennsylavania ambapo zaidi ya asilimaia 94 za kura zimehesabiwa Trump ana asilimia 49.7 na Biden 49.0. Arizona ambako asilimia 90 zimehesbabiwa Trump ana asalimia 48.5 na Biden 50.1, Georgia asilimia 99 zimehesabiwa Trump asilimia 49.4 na Biden asilimia 49.4 na Nevada kati ya asilimia 89 zilizohesabbiwa Trump asilimia 48.5 na Biden 49.4.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Heiko Maas amezitaka pande hasimu katika uchaguzi wa Marekani kuonesha ustahimilivu hadi matokeo kamili ya uchagu wao yapatikane, na kuongeza kuwa si wajibu kwao kuzidisha mvutano. Akizungumza na chombo kimoja cha habari cha Ujerumani, alisema Marekani ni zaidi ya onyesho la mtu mmoja, na kwamba yeyote anaemwaga mafuta kwenye moto kama inavyoonekana kipindi hiki, anafanya vitendo visivyo vya uwajibikaji.

Soma zaidi:Ushindi wanukia kwa Biden

Katika taarifa yake hiyo ya kwanza kabisa kuhusu uchaguzi wa Marekani amenukuliwa akisema "Sasa ni muda wa kuwa watulivu kabisa, mpaka matokeo yatakapo tolewa." Zaoezi la kuhesabu kura katika uchaguzi huo wa Novemba 3, linaendelea, huku bado ikionekana kuwa na mchuano mkali kabisa ambapo wagombea wa urais wakijongeleana kwa karibu zaidi. Trump ameanzisha madai kadhaa katika baadhi ya majimbo ya uchaguzi kwa lengo la kupunguza kasu ya mpinzani wake Joe Biden, hatua ambayo imezusha hali ya wasiwasi katika taifa hilo kubwa kabisa duniani.