Tunatumia 'cookies' ili kuboresha huduma zetu kwako. Maelezo zaidi yanaweza kupatikana katika sera yetu ya faragha.
Chama cha Democratic cha Marekani ni mmoja ya vyama viwili vikubwa zaidi nchini humo. Wafuasi wa chama hiki wanajulikana kama Wademocrat.
Katika ukurasa huu utapata maudhui mbalimbali za DW kuhusu chama cha Democratic na Wademocrat.
Jeshi la Ukraine limesema kuwa shambulizi la anga la Urusi limeushambulia mji wa bandari wa Odesa na kuharibu makaazi ya kitalii, ambapo watu watatu wamejeruhiwa.
Marekani imetangaza kutoa msaada wa fedha dola milioni 150 ili kusaidia nchi za Jumuiya ya Mataifa ya Kusini Mashariki (ASEAN) kuimarisha usalama wa baharini na miundombinu ya afya.
Waziri wa mambo ya kigeni wa Urusi Sergey Lavrov amefanya ziara ya kushtukiza nchini Oman na kufanya mazungumzo na maafisa wa nchini humo kuhusiana na vita vinyoendelea nchini Ukraine.
Chama cha kihafidhina cha Ujerumani cha Christian Democratic Union, CDU kimeshinda uchaguzi katika jimbo la kaskazini la Schleswig-Holstein.
Rais Joe Biden ametangaza shehena mpya ya silaha za Marekani yenye thamani ya dola milioni 150 kwa ajili ya kuisaidia Ukraine kupambana na Urusi.
Maandamano yamefanyika Marekani, baada ya kuvujishwa kwa waraka wa maoni, unaoashiria kuwa mahakama ya juu ya nchi hiyo inaweza kufuta sheria ya mwaka 1973 iliyohalalisha uavyaji wa mimba nchini humo.
Urusi imefanya mashambulizi mapya katika bandari muhimu ya Odessa wakati ambapo Marekani imetahadharisha kuwa Urusi inajiandaa kuzingira rasmi maeneo yanayopiganiwa kwa sasa mashariki mwa Ukraine.
Mji mkuu wa Ukraine umetikiswa kutokana na mashambulio makali yaliyofanywa na majeshi ya Urusi wakati Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akifanya ziara nchini humo.
Uchunguzi uliofanywa jimboni Minnesota nchini Marekani umebaini kwamba maafisa wa polisi katika mji wa Minneapolis wana chembe chembe za "ubaguzi wa rangi".
Urusi imeutuhumu muungano wa kujihami wa NATO kwa kile inachosema ni kuweka mazingira ya kuanza kwa vita vya nyuklia kwa kuipatia Ukraine zana za kivita.
Takriban watu watano wameuawa na wengine 18 kujeruhiwa katika shambulizi la roketi la Urusi mjini Vinnytsia. Huku Umoja wa Mataifa ukiongeza maradufu ombi lake la msaada wa dharura wa kibinadamu nchini Ukraine.
Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin ameanzisha mkutano wa masuala ya usalama na zaidi ya nchi 40 Jumanne nchini Ujerumani kwa kuelezea matumaini kwamba Ukraine inaweza kuishinda Urusi.
Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya, Ursula von der Leyen, na Waziri Mkuu wa India, Narendra Modi, wametangaza kuzinduliwa kwa Baraza maalum la kuimarisha Biashara na Teknolojia baina ya EU na India.
Ukraine imeutaka Umoja wa Mataifa kusimamia zoezi la kuwaondoa raia waliozingirwa kwenye eneo la kiwanda cha chuma katika mji wa Mariupol ambalo ni ngome ya mwisho ya wanajeshi wa Ukraine katika mji huo wa bandari.
Mawaziri wa ulinzi wa Marekani Lloyd Austin na wa Mambo ya Nje Antony Blinken walifanya ziara mjini Kyiv na kukutana na rais wa Ukraine Volodymir Zelensky na kuahidi msaada wa silaha ili kukabiliana na Urusi.
Maafisa wa Ukraine wamesema vikosi vya Urusi vilijaribu kuvamia kiwanda cha chuma kinachowahifadhi wanajeshi na raia mjini Mariupol katika jaribio la kusambaratisha upinzani wa mwisho majini Mariupol.