1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TRIPOLI.Mkutano wafanyika juu ya maswala ya uhamiaji

22 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCqQ

Zaidi ya wawakilishi 50 kutoka nchi za umoja wa ulaya na mataifa ya Kiafrika wanakutana mjini Tripoli nchini Libya katika mkutano wa siku mbili.

Mkutano huo utajadili maswala ya uhamiaji.

Huo ni mkutano wa kwanza wa aina yake unaotarajiwa kuzingatia maswala mbali mbali yanayohusu uhamiaji usio halali na uhamiaji halali na pia sheria zinazo walinda wakimbizi.

Mkutano huo unafanyika kutokana na wimbi kubwa la wahamiaji hasa kutoka bara la Afrika wanaojaribu kuingia barani ulaya katika harakati za kuukimbia umasikini ulio katika nchi zao.

Mamia ya wakimbizi hao wamezama au kufa kwa njaa katika safari zao za hatari kwa njia ya baharini.