THE HAGUE:Kesi ya Taylor kusikilizwa tena
20 Agosti 2007Matangazo
Mahakimu wanaohukumu kesi inayomkabili rais wa zamani wa Liberia Charles Taylor leo wanatarajiwa kutoa uamuzi juu ya lini kesi hiyo itaanza kusikilizwa tena baada ya watetezi wa mshtakiwa kuomba muda zaidi wa matayarisho. Watetezi hao wapya wa bwana Taylor wameomba kesi iahirishwe hadi tarehe 7 januari mwaka ujao.Taylor anakabiliwa na mashtaka ya uhalifu wa kivita.
Anadaiwa kuhusika katika vita vya nchini Sierra Leone ambapo watu wapatao laki moja na alfu 20 waliuawa .