TEHRAN:Rais wa Iran atembelewa na mwenzake wa Nicaragua | Habari za Ulimwengu | DW | 10.06.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

TEHRAN:Rais wa Iran atembelewa na mwenzake wa Nicaragua

Rais Mahmoud AhmedNejad amekutana na mwenzake wa Nicaragua Daniel Ortego ambaye amefanya ziara nchini Iran.

Rais AhmedNejad amesema anatumai nchi yake na Nicaragua zitashirikiana katika kuleta usawa na amani duniani.

Bwana Ortego anafanya ziara ya siku mbili Iran akisema analengo la kuimarisha uhusiano kati ya mataifa hayo mawili. Aidha rais huyo wa Nicaragua amesisitiza kwamba pamoja na kuimarisha uhusiano huo nchi yake inataka kushirikiana kwa karibu na Marekani.

Mwezi Januari rais wa Iran alikutana na Ortego wakati akiwa ziarani Amerika Kusini kwa minajili ya kutafuta washirika wenye msimamo sawa na nchi yake.

Rais AhmedNejad pia alikutana na mshirika wake wa karibu Hugo Chavez wa Venezuela,rais wa Ecuodor Rafael Correa na Evo Morales wa Bolivia wote wakiwa ni wakosoaji wakubwa wa sera za rais Bush wa Marekani.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com