TEHRAN: Iran yatishia hatua kali dhidi ya vikwazo | Habari za Ulimwengu | DW | 19.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

TEHRAN: Iran yatishia hatua kali dhidi ya vikwazo

Rais wa Iran Mahmaoud Ahmadinejad amesisitiza tena kwamba Tehran itachukua hatua kali ikiwa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa litaiwekea vikwazo Iran kuhusu mpango wake wa nyuklia.

Akihutubia mkutano wa hadhara uliohudhuriwa na malefu ya wafuasi wake mjini Kermanshah, Ahmadinejad alionya kwamba juhudi za kuzuia utafiti wa Iran wa nyuklia zitachukuliwa kama kitendo cha uchokozi.

Matamshi ya rais Ahmadinejad yanathibitisha onyo ambalo limekuwa likitolewa na taifa hilo la kiislamu.

Haya yanafuatia matokeo ya uchaguzi wa mwishoni mwa juma lililopita ambapo umaarufu wa rais Ahmadinejad unaonekana ukianza kupungua baada ya wanamageuzi kupata idadi kubwa ya kura katika baraza la mji wa Tehran.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com