Sudan yachunguza mauaji ya Mmarekani | Habari za Ulimwengu | DW | 02.01.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Sudan yachunguza mauaji ya Mmarekani

KHARTOUM:

Wakuu nchini Sudan wanawahoji walioshuhudia tendo la mauaji ya mwanadiplomasia wa Marekani hiyo alhamisi.

Mwanabalozi huyo-John Granville alipigwa risasi, pamoja na dereva wake wa kiSudan katika barabara moja mjini Khartoum.Wakuu wa Sudan baado wanasisitiza kuwa tukio hilo halikuwa la kigaidi lakini ubalozi wa Marekani unasema ni mapema mno kujua nia ya shambulio hilo.

Tukio hilo limekuja siku moja tu baada ya kikosi cha pamoja cha Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa kuanza kazi za kulinda amani katika mkoa wa Sudan wa Darfur.

Mwanadiplomasia huyo wa Marekani alikuwa anafanya kazi na shirika la maendeleo la Marekani la USAID

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com