1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Sudan kuwasajili tena wanajeshi na askari wastaafu

27 Mei 2023

Jeshi la Sudan limetoa wito siku ya Ijumaa kwa askari wa akiba na wanajeshi waliostaafu kusajiliwa tena huku kukiwa ili kuongeza nguvu katika jeshi, hatua ilio kosolewa vikali waangalizi wa kusitisha mapigano.

https://p.dw.com/p/4RsuB
Sudan Khartoum | Zeremonie zur Unterzeichnung eines Rahmenabkommens zwischen Militärherrschern und Zivilmächten
Picha: El Tayeb Siddig/REUTERS

Wito wa wanajeshi kujisajili tena kupitia kambi za jeshi zilizopo karibu yao, inatajwa kulenga kuimarisha jeshi la nchi hiyo katika vita hivyo vya kuwania madaraka na wanamgambo wa RSF.

Msemaji wa jeshi nchini humo amesema hatua hiyo ni hiyari kwa wanajeshi. Sheria iliyopo ya majeshi ya Sudan inasema,askari wastaafu watasalia kuwa askari wa akiba, hivyo wanastahili kuandikishwa upya.

Wakati tangazo hilo la jeshi linatolewa katika baadhi ya maeneomapigano ya hapa na pale ymeendelea kushuhudiwa kwa wiki nzima, ingawa waangalizi wa kisitisha mapigano Saudi Arabia na Marekani wamesema kulikuwa na uzingatiaji, lakini hatua za jeshi zinaweza kuashiria kuwa linajiandaa na mzozo wa muda mrefu.

Waakazi katika mji mkuu wa Khartoum ambao nao umelengwa na mashambulizi wameendelea kuteseka kutokana na kukosa nishati ya umeme,maji safi, huduma ya afya na mawasiliano.

Soma Pia:Marekani, Saudia wasema usitishwaji mapigano Sudan unaheshimiwa kwa kiwango fulani

Nyumba nyingi hasa katika maeneo ya mabwanyenye na maduka ya bidhaa za vyakula, viwanda vya chakula kama unga na mahitaji mengine muhimu kumeshuhudiwa uhalifu wa uporaji.

"Yote ni sehemu ya machafuko ya vita hivi," alisema Taysir Abdelrahim,ambae yupo nje ya nchi amegundua uporaji nyumbani kwake.

"Hata kama tungelikuwa Sudan,hakuna unachoweza kufanya".

Shirika moja linalosaidia watoto walio na saratani lilisemanalo, nyumba ya wageni inayofanyia kazi imevamiwa, ikiwa ni pamoja na vyumba vyake vya usalama na vya wagonjwa.

Jeshi lataka kuondolewa kwa mjumbe wa Umoja wa Mataifa Sudan

Kiongozi wa jeshi Abdel-Fatteh al-Burhan alimwandikia Katibu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres hapo jana akimtaka kumuondoa mjumbe wake Volker Perthes.

Vyanzo ndani ya jeshi havijaeleza kwa undani sababu za hitaji hilo, lakini Perthes, ambaye aliteuliwa mnamo 2021, alichangia kusukuma mbele ajenda ya kipindi cha mpito kuelekea utawala wa kiraia, ambao baadhi ya maafisa wa jeshi walipinga mchakato huo.

Mapigano bado ´yamechacha´ nchini Sudan

Umoja wa Mataifa kupitia msemaji wake Stephane Dujarric amesema, Katibu Mkuu amestushwa na wito huo wa kiongozi wa kijeshi na kuongeza kwamba Guterres anajivunia mjumbe huyo maalum.

Msaada wa kiutu katikati ya vita

Mapigano hayo yaliozuka mnamo mwezi April yamesababisha takriban watu 1.3 kukimbia makaazi yao, takriban 840,000 wakikimbilia katika maeneo salama ndani ya taifa hilo huku wengine wapatao 250,000 wakivuka mipaka na kuingia mataifa jirani, kulingana na Umoja wa Mataifa.

Wizara ya Afya imesema takriban watu 730 wamefariki dunia,ingawa kuna uwezekano mkubwa idadi hiyo ikawa ni kubwa, huku miongoni mwa waliofariki ni pamoja na watoto wadogo pamoja na wanawake

Taarifa ya wizara ya afya imeendelea kuongeza kwamba nusu ya watu wa Sudan wapatao milioni 49 wanahitaji msaada.

Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani USAID limesema nafaka za kulisha takriban watu milioni 2 kwa mwezi zitawasili kwa meli ingawaje haikuwekwa bayana ni lini hasa zitawasili.

Soma Pia:Marekani yaonya juu ya ukiukwaji wa makubaliano Sudan

Hata hivyo bado haijulikani ni kwa namna gani misaada mingine ya kiutu itawafikia wasudani wengine ambao usalama wao sio wa uhakiki.

Saudi Arabia na Marekanizimesema kwamba baadhi ya misaada ilifikishwa Khartoum siku ya Ijumaa, bila kutoa maelezo.Msalaba Mwekundu nyao imesema ilifanikiwa kupeleka vifaa katika hospitali saba.