1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Usitishwaji mapigano Sudan unaheshimiwa kwa kiwango fulani

Lilian Mtono
26 Mei 2023

Saudi Arabia na Marekani zimebainisha hatua zilizopigwa za kuheshimu makubaliano ya kusitishwa mapigano kwa muda mfupi na mipango ya shughuli za kiutu nchini Sudan.

https://p.dw.com/p/4Rqal
Sudan | Kämpfe in Khartum
Picha: AFP/Getty Images

Hata hiyo, mapigano ya hapa na pale kati ya jeshi la Sudan na wanamgambo wa RSF yameripotiwa saa chache zilizopita, na kuathiri utulivu uliokuwepo katika mji mkuu Khartoum.

Mashuhuda aidha wamesema mapigano yametokea leo katika jimbo la Magharibi la Darfur, ikiwa ni siku ya nne ya muafaka wa siku saba wa kuwekwa chini silaha uliosimamiwa na Marekani na Saudia. 

Marekani yaonya juu ya ukiukwaji wa makubaliano Sudan

Kwa mujibu wa taasisi ya Armed Conflict and Event Data Project, mapigano hayo yamewauwa watu 1,800 tangu yalipozuka Aprili 15.

Umoja wa Mataifa unasema zaidi ya Wasudan milioni moja wameyakimbia makazi yao na wengine 300,000 wamekimbilia nchi jirani.