1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSudan

Mapigano yaripotiwa Khartoum usiku wa kuamkia Jumatano

Grace Kabogo
24 Mei 2023

Mapigano kati ya majenerali hasimu nchini Sudan yameendelea usiku kucha kwenye maeneo ya mji mkuu, Khartoum.

https://p.dw.com/p/4RkHs
Sudan Konflikte Kämpfe
Picha: AFP

Mapigano hayo yamesikika siku ya pili ya makubaliano ya wiki moja ya kusitisha mapigano yaliyofikiwa ili kuruhusu upelekwaji wa misaada na kuweka mazingira ya kuwepo makubaliano ya kudumu.

Usitishaji huo wa mapigano unaofuatiliwa na Saudi Arabia na Marekani, pamoja na pande zinazohasimiana, umefikiwa baada ya wiki tano za vita mjini Khartoum na jimbo la magharibi la Darfur.

Wakaazi wa Omdurman wamesema kumekuwepo na majibizano ya risasi usiku wa Jumanne kwenye maeneo kadhaa.

Wamesema milio ya mizinga imesikika pia karibu na kambi ya jeshi ya Wadi Sayidna, nje kidogo ya Khartoum.

Wakati huo huo, Mkuu wa shirika la haki za binaadamu la Umoja wa Mataifa, Volker Turk, amesema kinachoendelea Sudan kinahuzunisha.