Shell yasaini mikataba ya mafuta, gesi na Venezuela
6 Machi 2026
Makubaliano hayo yamesainiwa ikiwa ni miezi michache tu baada ya Marekani kumpinduwa na kumteka nyara rais wake, Nicolas Maduro.
Shell imesaini pia mikataba ya kiufundi na kibiashara na kampuni ya uhandisi ya Venezuela, VEPICA, na kampuni ya huduma za mafuta ya Marekani, Baker Hughes.
Mikataba hiyo inafuatia mkutano kati ya Waziri wa Mambo ya Ndani wa Marekani, Doug Burgum, na rais wa mpito wa Venezuela, Delcy Rodriguez, wiki hii.
Burgum ni waziri wa pili wa Marekani kuitembelea Venezuela tangu Washington ilimpomteka nyara Maduro mwezi Januari.
Wa kwanza alikuwa waziri wa nishati, Chris Wright, aliyekuwa Caracas mwezi uliopita.
Shell imekuwa na miradi ya muda mrefu nchini Venezuela lakini ilitatizika kutokana na kubadilika kwa sera ya Washington kuelekea Caracas.