1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Scholz kutembelea maeneo yaliyoathiriwa na mafuriko Bavaria

3 Juni 2024

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz na Waziri wa Mambo ya Ndani Nancy Feaser wanatarajiwa kuzuru maeneo yaliyoathirika kwa mafuriko katika jimbo kusini la Bavaria.

https://p.dw.com/p/4gZXb
Mafuriko|Bavaria|Ujerumani
Athari za mafuriko katika jimbo la kusini mwa Ujerumani la Bavaria.Picha: Bernd März/IMAGO

Mamlaka ya mji wa Regensburg imetangaza hali ya dharura baada ya kina cha maji katika Mto Danube kufikia mita 5.8.

Idara inayohusika na utoaji wa Taarifa za Mafuriko katika jimbo hilo la Bavaria, imesema mto huo uliendelea kujaa na kufikia kina cha mita 5.9 kwenye mji wa Regensburg, majira ya saa moja asubuhi hii leo.

Mji wa Regensburg, ulioko kaskazini mwa jiji la Munich ni mwingine miongoni mwa miji kadhaa katika jimbo la Bavaria iliyotangaza hali ya dharura baada ya kukabiliwa na mvua kubwa, huku idara ya Hali ya Hewa ikitahadharisha juu ya kuendelea kunyesha mvua zaidi.